Header Ads

Polisi Wakwama Kumhoji Tundu Lissu

Jeshi la Polisi limekwama kumhoji Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), akiwa hospitalini Nairobi, Kenya baada ya kiongozi huyo kusema kwamba polisi wa Tanzania hawawezi kumhoji akiwa nchini Kenya au kwingineko nje ya mipaka ya nchi.

Kauli ya Lissu imekuja siku 10 tangu Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, kuiambia Nipashe kuwa wametuma askari wawili kwenda Nairobi kuchukua maelezo ya Lissu, baada ya Mbunge huyo kukubali kuhojiwa.

"Hadi sasa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania hajamwomba Mwanasheria Mkuu mwenzake wa Kenya ruhusa ya mimi kuhojiwa na Polisi wa Kenya juu ya shambulio hilo kama inavyotakiwa na sheria husika za nchi yetu," amefafanua Lissu ambaye ni mwanasheria kwa taaluma.

Aidha kwa upande wa IGP Sirro Alipoulizwa maoni yake juu ya kauli hiyo ya Lissu kuwa polisi hawawezi kumuhoji nje ya mipaka ya nchi, aliiambia Nipashe “Mimi sina jibu.”

Wiki iliyopita, IGP Sirro alisema ametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kuwapata dereva na mlinzi wake.

“Tumetuma watu wetu kwenda kuchukua maelezo yake (Lissu). Mwanzo tuliomba kwenda lakini chama (Chadema) walikataa. Juzi tumesikia wamesema wapo tayari". Sirro

Allifafanua kwamba  lengo kubwa ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili kurahisisha upepelezi wa tukio lenyewe.

No comments:

Powered by Blogger.