Header Ads

Zijue sheria 17 za mchezo wa soka duniani


Kuna utata wa kwamba nani aliyegundua mpira wa mchezo huu lakini haipingiki kwamba huu ni mchezo maarufu zaidi na unaopendwa na watu wengi zaidi duniani kwa sasa.
Kila msimu mpya, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hutoa mabadiliko ya “Sheria za Mchezo” zinazoelezea kiundani taratibu za mchezo huo. Zifuatazo ni Sheria 17 za mpira wa miguu.
Sheria #1: Uwanja
Kuna vipimo maalumu vya viwanja wa mchezo wa soka, viwanja vidogo na vikubwa kadhalika. FIFA inasema kwamba katika mashindano ya mchezo wa soka wenye timu za wachezaji 11 kila moja, urefu wa uwanja unatakiwa uwe kati ya mita 100 na mita 130 na upana wake uwe kati ya mita 50 na 100.
Kuna nafasi 11 za wachezaji kwenye uwanja wa mpira wa miguu lakini zote zinaweza kuwekwa kwenye makundi makuu manne. Kwenye michezo midogo, idadi ya wachezaji kwenye kila timu inaweza kupungua lakini nafasi hizi zinabaki kama zilivyo. Nafasi hizi kwenye mchezo wa soka ni Golikipa, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji.
Sheria #2: Vipimo vya mpira
Mzingo (mzunguko) wa mpira wa miguu hautakiwi kuzidi kipimo cha inchi 28 (sawa na sentimita 70) na hautakiwi kupungua inchi 27 (sawa na sentimita 68).
Mpira saizi namba 5 ambao unatumiwa na watu kuanzia umri wa miaka 12 na zaidi una umbo la duara, na unatakiwa utengenezwe kwa ngozi au kwa kitu chochote kitachofaa.
Uzito wa mpira hautakiwi kuzidi gramu 450 na usipungue gramu 410 mchezo husika unapoanza.
Ujazo wa mpira unatakiwa kuwa kati ya gramu 0.6 hadi 1.1 za sentimita za ujazo kwa mchezo utakaochezwa nchi kavu.
Sheria #3: Idadi ya wachezaji
Mechi hujumuisha timu mbili ambazo kila moja haitakiwi kuzidi wachezaji 11 ndani ya uwanja kwa wakati mmoja ambapo mmoja wapo ni golikipa. Mchezo hauwezi kuruhusiwa kuanza iwapo timu yoyote itakuwa na wachezaji pungufu ya saba.
Kwenye mashindano rasmi yanayoratibiwa na FIFA, idadi ya wachezaji wanaoruhusiwa kubadilishwa ni watatu. Sheria za mashindano lazima zieleze idadi ya wachezaji wanaoruhusiwa kubadilishwa kuanzia watatu na isizidi saba.
Sheria #4: Vifaa vya wachezaji
‘Sheria za Mchezo’ kwa mujibu wa FIFA zinasema kwamba wachezaji hawaruhusiwi kutumia vifaa vyovyote au kuvaa chochote cha hatari kwake au kwa wachezaji wenzake (na hii inajumuisha vito vya madini).
Vifaa vya kawaida kwa mchezaji ni pamoja na jezi au fulana (ya mikono mirefu au mifupi), kaptura, soksi, kilinda ugoko na viatu.
Timu mbili zinazoshindana zinatakiwa kuvaa nguo za rangi tofauti ili waweze kujitofautisha dhidi ya wapinzani wao, dhidi ya muamuzi mkuu na dhidi ya wasaidizi wa waamuzi.
Sheria #5: Muamuzi mkuu wa mchezo
Muamuzi wa kati ana mamlaka ya mwisho ya kusimamia Sheria za mchezo na uamuzi atakaoutoa utakuwa wa mwisho.
Muamuzi wa kati anadhibiti mchezo kwa kushirikiana na wasaidizi wawili, na kama itabidi – msaidizi wa nne. Baadhi ya majukumu ya muamuzi ni kuhakikisha kuwa mpira na vifaa vya wachezaji vinakidhi mahitaji ya mchezo,  kuangalia muda na kusimamisha mchezo pindi sheria za mchezo zinapovunjwa.
Sheria #6: Wasaidizi wa muamuzi mkuu wa mchezo
Katika mchezo wa soka, kunatakiwa kuwa na wasaidizi wawili wa muamuzi wa kati na kazi yao ni kuamua endapo mchezaji amezidi upande wa timu pinzani, mipira ya kurusha na kumsaidia muamuzi wa kati kufanya maamuzi. Wanatakiwa kushika bendera muda wote kwa ajili ya kutoa ishara ya maamuzi yao na wanatakiwa muda angalia mistari ya pembeni ya uwanja na golini na kuinua bendera iwapo mpira utapovuka mistari hiyo kuashiria kama mpira unatakiwa kurushwa, kupigwa kutokea golini.
Sheria #7: Muda wa mchezo
Mchezo unatakiwa kuwa na vipindi viwili vya dakika 45 kila kimoja, labda ikiwa timu hizo mbili pamoja na muamuzi watakubaliana tofauti kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Kipindi cha mapumziko kati ya kipindi cha kwanza na cha pili hakitakiwi kuzidi dakika 15 na unaweza kubadilishwa kwa kumshirikisha muamuzi wa kati. Muamuzi anaweza kuongeza muda kutokana na muda utakaotumiwa wakati wa: kubadilisha wachezaji, yanapotokea majeruhi, kuangalia majeruhi, kumuondoa uwanjani mchezaji aliyejeruhiwa, muda uliopotezwa kwa makusudi au kwa sababu nyingine yoyote. Mechi ambayo haijachezwa inatakiwa kurudiwa labda iwapo sheria za mashindano husika zinapotaka vinginevyo.
Sheria #8: Kuanza na kuendelea kwa mchezo baada ya kusimamishwa
Mpira utaanza katikati ya uwanja wakati wa:
– Kuanza kwa mchezo
– Kama goli limefungwa
– Kuanza kwa kipindi cha pili
– Kuanza kwa vipindi vya ziada baada ya muda rasmi kumalizika
Sheria #9: Mpira kuwa nje ya mchezo
Mpira upo nje ya mchezo ikiwa:
– Mpira wote unapovuka mstari wa goli au mistari ya pembeni
– Mchezo unaposimamishwa na muamuzi
– Mpira utahesabika kuwa mchezoni kwa wakati wote ikiwemo:
-Kama utarudi uwanjani baada ya kugonga nguzo za pembeni ya goli, nguzo ya juu ya goli au bendera ya kwenye kona na ukarudi au kubaki ndani ya uwanja
-Utapomgonga muamuzi wa kati au muamuzi msaidizi mchezo unapoendelea
Sheria #10: Jinsi ya kuhesabu magoli yanayofungwa
Magoli yanayofungwa:
Goli litahesabiwa halali ikiwa mpira wote utavuka mstari wa golini uliopo katikati ya nguzo tatu za goli, ilimradi usiwepo ukiukwaji wa sheria kama kuzidi kwa mchezaji, mchezaji kuchezewa vibaya au kushika mpira.
Timu itayofunga magoli mengi zaidi ya mpinzani wake ndiyo itatangazwa mshindi wa mchezo huo. Kama mpaka mwisho wa mchezo idadi ya magoli yaliyofungwa kati ya pande mbili italingana, matokeo ya mchezo huo yatakuwa ni sare.
Kama sheria za mashindano zinahitaji mshindi apatikane, matokeo ya kupata mshindi huyo yatapatikana kutokana na moja kati ya njia zifuatazo:
– Sheria ya goli la ugenini
– Muda wa ziada
– Mikwaju ya penati
Sheria #11: Mchezaji anapootea/kuzidi
Mchezaji atahesabika kuwa amezidi kama atalikaribia goli la timu pinzani zaidi ya mpira na mlinzi wa mwisho lakini ni pale tu atakapokuwa kwenye nafasi hiyo akiwa upande wa nusu ya timu pinzani uwanjani.
Sheria inasema kwamba kama mchezaji amezidi na mpira ukapelekwa kwake na ukaguswa na mchezaji wa timu yake, anaweza kuamua kuuacha kana kwamba hayupo mchezoni ili mwenzake aendelee kuucheza.
Sheria #12: Makosa na nidhamu mbaya
Sheria za mchezo zinawekwa na Shirikisho la mchezo wa soka ulimwenguni (FIFA). Kitabu rasmi cha muongozo wa Shirikisho hilo kina jumla ya kurasa 140 ambacho kinajumuisha maelezo ya kina kuhusu kila aina ya kosa, madhambi na taratibu za mchezo.
Kwa ufupi kabisa, yafuatayo ni baadhi ya makosa mbalimbali yatayomsababisha mwamuzi wa mchezo kupiga filimbi yake, kusimamisha mchezo na pia kutoa adhabu kama ataona inafaa kama ilivyoelezwa na FIFA:
Adhabu ya mpira wa kupigwa moja kwa moja
Inapigwa pindi mchezo unapoendelea baada ya muamuzi kusimamisha kwa muda kutokana na kumpiga teke au kujaribu kumpiga teke mpinzani, kujaribu au kumuangusha mpinzani, kumrukia mpinzani, kujaribu au kumshambulia mpinzani, kumsukuma mpinzani.
Mpira wa adhabu ya moja kwa moja pia unatokana na kufanyika makosa kama: kumuangusha mpinzani anayeufata mpira na kumgusa mchezaji wa timu pinzani kabla ya kuugusa mpira, kumshika mpinzani, kumtemea mate mpinzani, kushika mpira kwa makusudi (isipokuwa kwa golikipa akiwa ndani ya eneo la penati).
Penati
Penati inatolewa kama lolote kati ya makosa hayo yaliyotajwa hapo juu litafanywa na mchezaji akiwa ndani ya eneo la penati la timu yake bila kujali mpira ulikuwa wapi – sharti pelee ni kwamba mpira huo unatakiwa uwe mchezoni kwa wakati huo.
Baada ya muamuzi kutaka adhabu ya penati ipigwe, mchezaji mmoja anaruhusiwa kupiga mpira huo kuelekea golini kwa mpinzani wake kwa lengola kufunga (na mlinzi pekee wa kuzuia anatakiwa kuwa golikipa wa timu pinzani anayetakiwa kusimama kwenye mstari wa golini) ambapo mpira utawekwa kwenye alama iliyo umbali wa mita 12 kutoka kwenye mstari wa goli.
Adhabu ya kupiga mpira isiyo ya moja kwa moja
Adhabu hii inapewa kwa timu pinzani ikiwa golikipa akifanya moja ya makosa yafuatayo ndani ya eneo lake la penati: akitembea zaidi ya hatua nne mpira ukiwa mikononi mwake kabla hajauachia, ataposhika tena mpira baada ya kuuachia alipokuwa ameushika (na ukawa haujaguswa na mchezaji yeyote), akigusa mpira kwa mikono yake baada ya kurudishwa kwake na mchezaji wa timu yake, akigusa mpira kwa mikono yake baada ya kurushwa moja kwa moja kutoka kwa mchezaji wa timu yake.
Adhabu hii pia itatolewa kwa timu pinzani iwapo mchezaji, kwa mujibu wa atavyoona muamuzi, kuwa amefanya kosa lolote kati ya haya yafuatayo: kucheza kiasi cha kuhatarisha wachezaji wengine, kumzuia mchezaji wa timu pinzani, kumzuia golikipa wa timu pinzani asiachie mpira ulio mikononi mwake, atapofanya kosa lolote ambalo halijaorodheshwa ambalo litasababisha mchezo kusimamishwa ili kumuonya au kumtoa mchezaji aliyefanya kosa hilo.
Kadi ya njano
Baada ya kuruhusu kupigwa kwa adhabu ya mpira wa adhabu au penati, mwamuzi anaweza kuendelezea kumuadhibu mchezaji aliyeonesha utovu wa nidhamu kwa kumuonesha kadi ya rangi ya njano au nyekundu.
Kadi ya njano
Mchezaji anaonywa kwa kuoneshwa kadi ya njano kama akifanya kosa lolote kati ya haya yafuatayo:
akionesha tabia isiyo ya kimichezoakikataa maamuzi yaliyotolewa kwa maneno au vitendoakirudia kukiuka sheria za soka mara kwa maraakichelewesha kuendelea kwa mchezoakishindwa kusimama umbali unaotakiwa wakati timu yake ikipigiwa mpira wa adhabu ya mpira wa kona au mpira wa kupiga moja kwa mojaakiingia uwanjani bila kuruhusiwa na mwamuziakitoka uwanjani kwa makusudi bila kuruhusiwa na mwamuzi
Kadi nyekundu
Mcheaji atatolewa nje ya uwanja baada ya kuoneshwa kadi ya rangi nyekundu kama akifanya moja ya makosa yafuatayo:
akiwa amecheza vibaya kwa mchezaji kwingineakithibitika kufanya au kusababisha vuruguakimtemea mate mchezaji wa timu pinzani au mtu yeyoteakimchezea vibaya mchezaji wa timu pinzani itayosababisha kumnyima nafasi ya kufunga goli au anapokuwa na nafasi ya wazi kabisa ya kufunga golikwa kushika mpira kwa makusudi (isipokuwa kwa golikipa anapokuwa kwenye eneo lake)akimzuia kwa makusudi mchezaji wa timu pinzani aliye kwenye nafasi ya wazi wa kwenda kufunga goli kwa kosa linaloweza kuadhibiwa kwa mkwaju wa penati au mpira wa adhabu ya moja kwa mojaakitoa lugha chafu ya kutukana, kudhalilisha, kudharau au kubagua wengineakionywa kwa mara ya pili ndani ya mchezo mmoja
Sheria #13: Mpira wa adhabu
Mpira wa adhabu waweza kupigwa moja kwa moja au kwa kupena pasi na mpira ni lazima uwe umetulia wakati wa kuupiga kutekeleza adhabu hii. Mpigaji haruhusiwi kuugusa mpira huo kwa mara ya pili kabla haujaguswa na mchezaji mwingine.
Mpira huru kwenye soka unaweza kupigwa moja kwa moja kuelekea kwenye goli la mpinzani au kwa wachezaji wa timu pinzani kuweka ukuta (wakijipanga umbali fulani kabla mpira huo kupigwa ambapo hawaruhusiwi kuugusa kabla haujapigwa) wa ulinzi na mpira unatakiwa uwe umetulia wakati wa upigaji wa mpira huo. Mpigaji hatakiwi kuugusa kwa mara ya pili mpira huo kabla haujaguswa na mchezaji mwingine.
Sheria #14: Adhabu ya penati
Mchezaji anaruhusiwa kusitasita akiwa anakimbia kuelekea kupiga adhabu ya penati kwa nia ya kumhadaa golikipa wa timu pinzani. Lakini, kusita kupiga mpira baada ya kumaliza kukimbia kinahesabika kuwa ni kitendo kisicho cha kimchezo ambapo mchezaji aliyefanya hivyo ni lazima aonywe na muamuzi.
Maandalizi ya penati
Muamuzi lazima ahakikishe yafuatayo kabla penati haijapigwa:
– mpigaji ameshachaguliwa
– mpira umewekwa kwa usahihi juu ya alama ya kupigia penati
– golikipa amesimama kwenye mstari wa golini na amuelekee mpigaji
Wachezaji wengine wote waliopo uwanjani wanatakiwa kuwa:
– Nje ya eneo la penati – na nje ya mchoro wa upinde unaochorwa kwa nje ya eneo la penati
– Behind the ball.
Sheria # 15, 16 na 17: Mpira uliotoka nje ya uwanja (wa kurusha, mpira unaopigwa kutoka golini na adhabu ya kona)
Endapo mpira utatoka nje ya mistari inayoonesha alama za uwanja, mpira huo unatakiwa urushwe na mchezaji kutoka timu ambayo si mchezaji wake aliyegusa mpira huo kwa mara ya mwisho. Iwapo mpira wote utavuka mstari wa pembeni mwa goli, adhabu ya kona au golkiki vitaamriwa, kutegemea ni mchezaji wa timu ipi amegusa mpira kwa mara ya mwisho kabla mpira kutoka. Kama mchezaji wa mwisho kuugusa ni wa timu inayoshambuliwa, adhabu ya kona inatakiwa kutolewa. Kama mchezaji wa timu inayoshambulia aliugusa mpira mara ya mwisho kabla haujatoka, mpira wa golkiki unatakiwa kupigwa imechambuliwa na kuletwa kwenu na mchambuzi wako Anthony MALEGES

42 comments:

  1. Replies
    1. Ni nzuri sana Ila baadhi ya marefa wameshindwa zifuata.

      Delete
  2. Hongera Sana kwa uchambuzi wako mahili kwelikweli

    ReplyDelete
  3. Je eti mpira wakulushwa kma umerushwa af umeingia gorini bila kuguswa ni gori ama si gori

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio goli. Kama mpira umerushwa na timu pinzani, itakuwa golikiki, kama ulirushwa na timu hiyo hiyo itakuwa kona!

      Delete
    2. Hapa nivipi ju mm pia sielewi

      Delete
  4. Adhabu gan itatolewa endapo golikipa atashika Mpira alorudishiwa na mwenzake

    ReplyDelete
  5. Je!? Kadi nyekundu inaweza futwa Kama mchezaji alionewa.

    ReplyDelete
  6. Replies
    1. Nashukuru Sheria zipo vizuri baada ya kusoma Sheria zote 17 Nina uwezo wa kuchezesha mpila wa miguu

      Delete
  7. In short it's good football rules!!

    ReplyDelete
  8. Napenda kusomea uamuzi je nuvigezo vipi unatakiwa kua navyo?

    ReplyDelete
  9. Nice. I like it. Great thanks🙏

    ReplyDelete
  10. Replies
    1. Je Kama mchezaji akiji funga hatrack anaruhusiwa kuondk na moir

      Delete
  11. Unajua mpiraa ugali nin kwambaa leta ungaa songaa

    ReplyDelete
  12. Swali langu:je mchezaji anapo piga mwamuzi Kwa makusudi,mpira usimama na timu pinzani kupewa ushindi ama mpira uendelea na mchezaji kupewa card nyekundu,ama mchezaji upewa card nyekundu na team kupoteza ushinda na ata kuwa disqualified?

    ReplyDelete
  13. Fafanua vizur kuhusu sheria namba 15,16,17

    ReplyDelete
  14. Nimesoma... Sheria 15-17 ?? Haziko wazi

    ReplyDelete

Powered by Blogger.