Header Ads

SAFARI YA MAPENZI

Mapenzi ni kama safari, Yaani unatoka nyumbani peke yako ukielekea stand ya bus, unafika hapo unakutana na mtu mnaanza kuongea na kufahamiana, Katika mazungumzo unatambuwa mko safari moja... Mwendo wa safari hiyo ni mrefu, Kuna mahala mlisimama kuchimba dawa, Kuna mahala mlisimama kula chakula na kuna wakati dereva alichoka na kusema ABIRIA TUPUMZIKE KIDOGO! Wakati mkiendelea na safari hiyo ambayo ndani yake ina furaha na amani maana umesafiri na mtu ambaye moyoni mwako unahisi unampenda... Lakini kama wasemavyo wahenga "MOYO WA MTU NI CHAKA" ni ngumu sana kujuwa anayoyafikiria mwenzio, Ghafla bus linasimama kwa muda na Mwenzio anakuomba ashuke kuna kitu anunue, Nawe bila kujuwa unasema sawa nenda kanunue, Mpaka bus linaondoka hajarudi na unapaza sauti kusema kuna abiria mwenzangu mnamuacha, Dereva anapiga honi lakini mwenzio asiweze kutokea, Tayari ushamzoea, Tayari umempenda, Tayari ameweka alama moyoni mwako, Tayari ushamjenga rafiki yako lakini ndo hivyo umebaki peke yako, Huzuni ni kubwa maana hujui alishuka akakutwa na kitu gani huko? Hujui ndugu yake wala huna acces ya kujuwa lolote juu yake, Lakini kabla ya kuumia jiulize jambo hili JE WAKATI ANAPANDA BUS HILO UNA HAKIKA GANI KAMA SAFARI YAKE ILIKUWA YA HUKO UENDAKO WEWE? Pengine alipanga kushukia kituo hicho, Na wakati anapanda bus alipendezwa nawe tu ndo maana akataka kukupa kampani lakini masikini ya MUNGU hakuwa na sababu ya kuendelea zaidi ya alipokuwa amepanga kushuka, Nini maana ya ujumbe huu;
USIMPE MTU NAFASI NDANI YA MOYO WAKO kabla hujajuwa anakuja kwako kwa mtazamo upi? Wako watu wao hupanga KUWA NA MAHUSIANO ILI KUONDOA STRESS kitu ambacho kwako kitakuangamiza moyo kwani wewe hutajuwa hilo na badala yake UTAJIACHIA UNYAYO HADI UTOSI kumbe unalambishwa mabaki ya uji, Usimpe mtu nafasi akaujuwa UDHAIFU wako, Wengi hutumia udhaifu wako kukuchapa na mwisho wake WEWE NI KUWA MHANGA WA PENZI LAKE... Simama katika msitari ujue kwamba MAPENZI yanaumiza sana lakini pia yanaharibu mtazamo wa ki fikra mwisho wa siku ni wewe kukosa FURAHA NA AMANI katika dunia hii, Mungu hakutuumba kwa mfano wake kwa bahati mbaya maana kama ni MAPENZI kila kiumbe hufurahia kwa namna yao, Kwani hujawahi ona MENDE WAKISHIRIKI KI MWILI?🐞
Kwanini sisi tunafurahia zaidi yao? Kwa sababu tulipewa upendeleo na ndo maana KWA KUTOKUJUWA KWETU MAANA YA UBIN ADAM WETU tumekuwa hatuhurumiani, Mpe MOYO WAKO mtu ambaye anajuwa kuwa WEWE NI MUHIMU KWAKE! Ukikosea ukampa MOYO wako mtu asiyejitambuwa wallah UNAWEZA KUOKOTA MAKOPO laaa uachwe na maradhi ambayo mpaka unakufa utakuwa unajuwa yeye ndiye chanzo, Yanini Mateso na dunia yenyewe ishakwisha hii tunailazimisha tuuu? Be strong enough 💪🏽
#MAKTABATZ_kasema_ila_sio_sheria.

No comments:

Powered by Blogger.