Header Ads

Magolikipa wanaoshikilia rekodi pamoja na David de Gea

Arsenal walishambulia lango la Manchester United mara 15 Jumamosi, lakini hawakufanikiwa kutikisa wavu isipookuwa mara moja tu - kikwazo chao David de Gea.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alisema uchezaji wa golikipa huyo wake ulikuwa "bora zaidi duniani".
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia alikiri kwamba Mhispania huyo alciheza kwa ustadi mkubwa na kwamba "alikuwa ndiye mchezaji bora wa mechi kwa mbali sana".
Uchezaji wake ulikuwa muhimu sana kwani uliwasaidia kulaza Arsenal 3-1 - na pia ulifikia rekodi Ligi ya Premia.
 Hatua yake ya kuzima makombora 14 inamfanya kushikilia rekodi ya kuzuia makombora mengi zaidi mechi moja Ligi Kuu England pwa pamoja na mlindalango wa zamani wa Newcastle Tim Krul na kipa wa zamani wa Sunderland Vito Mannone.


Waliozuia makombora mengi zaidi mechi moja EPL tangu Agosti 2003 (Opta walipoanza kufuatilia data)



Kevin de Bruyne, kiungo wa kati wa Manchester City mwenye miaka 26, alisaidia ufungaji wa bao mara ya nane msimu huu ligini.
Alisambaza mpira na kumuwezesha David Silva kufunga mechi ambayo walilaza West Ham 2-1.
Amesaidia ufungaji wa mabao 35 ligini akiwa an City tangu awachezee mechi ya kwanza Septemba 2015.
Hakuna mchezaji mwingine ligi tano kuu za Ulaya (England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania) amesaidia ufungaji wa mabao mengi kama yeye. Amemwacha Mesut Ozil wa Arsenal kidogo.

Mabao ya kujifunga

 

Jumamosi, beki wa Brighton Lewis Dunk alijifunga kwa mara ya tatu msimu huu, na kuwasaidia Liverpool kulaza timu yake 5-1.
Ina maana kwamba amejifunga kila mechi tano. Rekodi hata hivyo inashikiliwa na beki wa zamani wa Charlton Richard Rufus ambaye alijifunga mabao matano katika mechi 99.



No comments:

Powered by Blogger.