Watoto sita kupatiwa matibabu ya moyo Israel
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka watoto sita wenye umri wa mwaka mmoja hadi 13 nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Katika safari hiyo wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana. Baada ya matibabu kukamilika wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano JKCI imeeleza licha ya Taasisi hiyo kutoa matibabu pia ina mkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.
Hili ni kundi la tano la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

No comments: