KINACHOTESA KWENYE MAPENZI NI MATARAJIO NA MTAZAMO WA PENZI HUSIKA!
Kinachotesa
kwenye MAPENZI NI MATARAJIO NA MTAZAMO WA PENZI HUSIKA! Kuacha ni ngumu
lakini ukithubutu ni USHINDI... Kuachwa ni hatari lakini ukiipokea hali
hiyo ni TIBA YA STRESS na yote hayo yanahitajiana kulingana na vile
ambavyo unapenda kuishi na FURAHA YAKO MWENYEWE! Na usijaribu kumshika
mtu ambaye yeye Mwenyewe amepanga akuondoke, akitaka kuondoka mwache
aende maana ukimzuia na hana mpango nawe
ITAKUGHARIMU... Je unalijuwa donda ndugu la MAPENZI? Donda la mapenzi
ni MAZOEA! Unajuwa kupenda kila mmoja anapenda vizuri tu, Lakini ili
uweze kudhihilisha pendo lako la ndani ni pale unapokuwa UMEMZOEA MTU
HUYO! Kama hujamzoea Mpenzi wako ni ngumu sana kuumia akiondoka, Wanao
umia juu ya Mapenzi ni wale ambao kwa hakika WAMEMZOEA MTU kiasi kwamba
hakuna siku ilokwenda bila kukutana, kuongea na kutumiana jumbe za
mahaba, Kwa maana hiyo ukitaka uishi salama kwenye mapenzi achana na
kumzoea mtu wako, Mazoea yanatesa hasa ukijitazama na kukumbuka zile
nyakati ambazo Mwenza wako aliishi nawe pembezoni mwa mbavu zako ama
alivyohusika kwenye Mambo yako muhimu WALLAH HUTAWEZA ni ngumu mno, Haya
mapenzi bwana yalitengenezwa mahala pabaya sana, Mapenzi yangekuwa
kwenye paji la uso nani angeteswa nayo? Maana ingekuwa rahisi kujuwa
USALAMA wako, Lakini bwana wangu weee MAPENZI YAMEJENGWA SIRINI...
Asikudanganye Mtu eti yeye Bingwa, Kila mmoja analia kwa aina ya kilio
chake ambacho kinamstahili, Elista mwenyewe naliaga juu ya wifi/shemeji
yenu HUU MCHEZO UNAHITAJI AKILI😎
#MAKTABATZ_kasema_ila_sio_she ria.
#MAKTABATZ_kasema_ila_sio_she
No comments: