Maandalizi sherehe ya miaka 56 ya Uhuru Yakamilika
Maandalizi
ya maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru yamefikia hatua za mwisho huku
Serikali ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na gwaride la mkoloni
litakalofanywa na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge alisema itakuwa ni mara ya kwanza kwa gwaride hilo la mkoloni kufanyika katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge alisema itakuwa ni mara ya kwanza kwa gwaride hilo la mkoloni kufanyika katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.
“Maandalizi
muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya uwanja na mahitaji mengine
muhimu yapo katika hatua za mwisho,” alisema DK Mahenge.
Alifafanua
kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride
maalumu la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini
na onyesho la makomandoo.
Nyinginie
ni kwata ya kimya kimya iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Onyesho la Jeshi la mkoloni kutoka Jeshi la Polisi.
“Watoto 225 kutoka shule za sekondari watashiriki katika gwaride hilo,” alisema.
Alisema lengo la Serikali kuwashirikisha ni kuwafundisha na kuwaridhisha tunu ya uhuru, uzalendo, umoja, mshikamano na utaifa.
Pia, kutakuwa na vikundi vya ngoma za asili kutoka Ruvuma, Kigoma, Zanzibar pamoja na kwaya kutoka Chunya mkoani Mbeya.
DK
Mahenge aliwasihi Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kupiga vita
rushwa na kufanya kazi kwa bidiii kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Pia,
aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na
kutoogopa mizinga itakayopigwa katika sherehe hizo kwasababu haina
madhara.
No comments: