Umati wamuokoa rais wa zamani wa Georgia kutoka kwa polisi Ukrain
Wafuasi wa rais wa zamani wa Georgia
Mikheil Saakashvili wamemoukoa kutoka kwa gari la polisi kwennye mji
mkuu Kiev baada ya kukamatwa kufuatia madai kuwa anasaidia kundi la
kigaidi.
Bw Saakashvili 49, aliutaka umati kumuandoa madarakani rais Petro Poroshenko ambaye ni mshirika wake wa zamani. Alipewa uraia wa Ukrain mwaka 2015 hatua iliyosababisha apoteze uraia wake wa Georgia.
Bw. Saakashvili amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bw. Poroshenko.
Anamlaumu rais kwa kushindwa kumaliza ufisadi. Bw Porokoshenko amekana madai kama hayo hapo awali.
Akiwa na pingu kwenye mkono mmoja na akizungukwa na mamia ya watu, Bw Saakashvili aliwashauri wafuasi wake kutembea kwenda kwa bunge la Ukrain.
"Ninawashauri kuanza maandamano ya amani ya kumuondoa madarakani Poroshenko. Msiogope," alisema kwa njia ya vipasa sauti.
Maafisa hawazungumzi lolote kufuatia kukombolewa kwa Bw Saakashvili. Mapema maafisa waliokuwa wamejifunika nyuso walimkamata Bw. Saakashvili, 49 kutoka nyumbani mwake.
Bw Saakashvili anashukiwa kwa kupokea msaada ya kufedha kutoka kwa kundi lenye uhusiano na rais wa zamani wa Ukrain Victor Yanukovich.
Bw. Saakashvile anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.
No comments: