Tundu Lissu atuma salamu wiki ya msaada wa sheria....Awataka Watanzania Wasichoke Kumuombea
Rais
wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ametumia
maadhimisho ya wiki ya msaada wa sheria kuwaomba wananchi kumwombea
apone na kurudi nchini aendelee kutoa mchango wake katika taaluma ya
sheria.
Lissu
tangu Septemba 7 amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya
anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi
akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma.
Akizungumza
leo Jumatatu Desemba 4,2017 katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa
sheria, mwakilishi wa TLS, John Seka amesema Lissu anawasalimia
wananchi.
“Rais
wa TLS, Tundu Lissu anawasalimia sana, anaendelea kupata nafuu ila
anawaomba Watanzania waendelee kumwombea ili apone haraka,” amesema Seka.
Amesema
Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ana hamu ya
kurudi nyumbani aendelee kutoa mchango wake wa kisheria kwa wananchi.
Kuanzia leo hadi Desemba 8,2017 wananchi wanapata fursa ya kupata msaada wa kisheria katika migogoro inayowakabili.
Seka
ametoa wito kwa wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam na mikoani kupata huduma ya msaada wa kisheria.
Amesema
baada ya wiki hiyo kumalizika, wananchi watatakiwa kufika ofisi za TLS
kupata msaada wa kisheria kwa kuwa hilo ni moja ya majukumu ya chama
hicho.
No comments: